Zuchu Apewe Heshima Yake, Avunja Rekodi Hii na Kumfikia Diamond Platnumz
Ni msanii @diamondplatnumz peke yake Tanzania mwenye wimbo wenye views zaidi ya milioni 50 YouTube ambao hajashirikiana na mtu. Wimbo huo ni Sikomi wenye zaidi ya views milioni 51 ambao ulitoka rasmi miaka mitatu nyuma
Kwa muda mfupi toka atambulishwe rasmi kwenye game ya Bongo Flava,msanii @officialzuchu amefanikiwa kufikisha views milioni 50 YouTube kupitia wimbo wake wa Sukari uliotoka miezi 6 nyuma ambao ameimba peke yake.
Hii ni ishara kuwa anaenda kuwa msanii wa kwanza Tanzania mwenye wimbo ambao si collabo wenye views nyingi YouTube kuliko msanii yeyote kwa miezi kadhaa mbele.👏👏
No comments