Header Ads

Header ADS

Taliban "Hatutangazi serikali mpya hadi Marekani iondoke Afghanistan"




Kundi la Taliban limesema kwamba halitotangaza serikali yake hadi pale Marekani itakapokamilisha kuviondoa vikosi vyake.
Vyanzo viwili ndani ya kundi hilo vimelieleza shirika la habari la AFP kuwa uundaji wa serikali na baraza la mawaziri hauwezi kutangazwa ikiwa bado kuna wanajeshi wa Marekani.

Awali kundi hilo limenukuliwa likisema kwamba halitokubali Marekani kurefusha muda wa mwisho wa Agosti 31 wa kuyaondoa majeshi yake na kuonya kwamba kufanya hivyo kutakuwa na athari kubwa.

Wakati huohuo msemaji wa muda mrefu wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid, amewataka Maimamu nchini humo kuwapa uhakikisho Waafghani juu ya usalama wao na kuondoa propaganda zisizo na misingi zinazoenezwa na Marekani juu ya Taliban


No comments

Powered by Blogger.