Gwajima Agomea Kiti na Kipaza Sauti Kilicho Andaliwa na Kamati
MBUNGE wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amekataa kutumia kipaza sauti (MIC) na kiti kilichokuwa kimeandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakati alipohudhuria kikao na kamati hiyo.
Gwajima ameitwa mbele ya kamati hiyo baada ya bunge kumtuhumu kwa mambo mbalimabli yakiwemo kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.
Kikao hicho kilipaswa kuanza saa saba mchana, lakini Askofu Gwajima alifika saa nane mchana na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza kwa kikao hicho. Hata hivyo kikao kimeanza majira ya saa 8:43 mchana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emanuel Mwakasasa amesema, Askofu Gwajima anahaki ya kuomba kubadilishiwa kiti pamoja na mic.
No comments