Header Ads

Header ADS

Mimba Ya Paula Yamchefua Kajala





RUMANSI kwamba mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Paula Paul au Paula Kajala kwamba amenasa mimba ya msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ zimemchefua ile mbaya mama wa binti huyo, Kajala Masanja.


Kwa mujibu wa kurasa za udaku, Paula alidaiwa kuonekana kwenye hospitali moja ya kishua wilayani Kinondoni akipima Ultra-Sound kuangalia kiumbe alichonacho tumboni kina hali gani.

 

Waliomuona Paula walidai kwamba, ana dalili zote za mimba kutokana na mabadiliko ya kimwili ikiwemo kuvimba mashavu na kurefuka shingo.Baadhi ya kurasa hizo zilimpongeza Kajala kwa kuwa anakwenda kuwa bibi baada ya kupata mjukuu.



Katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA, Kajala amesema kuwa, alichefuliwa mno na habari hizo na kwamba hazina ukweli wowote.Kajala anasema kuwa, hakuna ishu kama hiyo na mwanaye huyo hana mimba.

 

Kajala alikwenda mbali zaidi na kuchimba mkwara kwamba, endapo wasambazaji wa habari hizo wataendelea kumchafua mwanae, basi hatua za kisheria zitafuata.Paula na Rayvanny imekuwa ni ‘kapo’ inayofuatiliwa zaidi hivyo tetesi za mimba zimekuwa zikienea kwa haraka kama moto wa kifuu.




No comments

Powered by Blogger.