Mange Kimambi Asherehekea Mtandaoni Baada ya Mtoto Wake Kupata A zote High School
Ameandika Haya katika Ukurasa wake Instagram:
Nimeamka nna rahaaaaa…Jamani mwenzenu binti yangu anaanza degree yake ya sheria mwezi ujao at Durham University in UK. Kapata A zooooote A-level, yani kibongo bongo ni division 1 ya ukweli 🙌🙌🙌. Najihisi kama nimemaliza kulea sina wasiwasi tena. Hawa wakiume acha wawatie mimba mabinti zenu, Im kidding
Ambao bado mnalea watoto wa kike, Mungu awasaidie kama alivyonisaidia mimi. Ila kina Kenzo wakiwapitia wabinti zenu mi simo
Hapa bank account yangu inakaribia kufika zero balance maana kila nikikumbuka Bhoke wangu anaingia chuo kikuu namtumia vipaundi. Na ma aunty zake kina @the_ironlady1976 wamenitumia $$ nimtumie mtoto wao. Mwanangu Cassandrah hela zako from kina Aunty zinakujaaaaa. Umejua kunitoa kimasomaso mamako. Acha nikate viuno tu.
No comments