IGP Simon Sirro "Chadema Wanamuona Mbowe Malaika Hawezi Kufanya Kosa"
“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”
“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”
“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”
“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”
“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna” ——— asema IGP Simon Sirro akiongea na Waandishi wa Habari leo Dar es salaam.
No comments