China: Sera ya watoto watatu yapitishwa rasmi kuwa sheria
China imefanya marekebisho rasmi kwa sheria zake ili kuwaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, ili kuongeza kiwango cha kuzaliana.
Kanuni hiyo ilikuwa moja kati ya kadhaa zilizopitishwa Ijumaa kwenye mkutano wa wabunge wa bunge la kitaifa National People Congress (NPC).
Maelezo juu ya sheria yenye utata ya kupambana na vikwazo dhidi ya Hong Kong, ambayo wafanyabiashara wengi walihofia ingewaweka katika wakati mgumu, pia ilitarajiwa.
Lakini vyombo vya habari vya Hong Kong viliripoti Ijumaa kuwa uamuzi huo umecheleweshwa.
China ilitangaza mnamo mwezi Mei kuwa itawaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, katika mabadiliko makubwa ya sera.
Uamuzi huo sasa umepitishwa rasmi kuwa sheria, pamoja na maazimio kadhaa ambayo yalilenga kuongeza kiwango cha kuzaliana na "kupunguza mzigo" wa kulea mtoto, limesema shirika la habari la Xinhua.
Hii ni pamoja na kufuta "ada ya uendelezaji jamii" - adhabu ya kifedha kwa wanandoa hulipwa kwa kuwa na watoto zaidi ya idadi iliyoidhinishwa, kuhimiza serikali za mitaa kutoa likizo ya wazazi, kuongeza haki za ajira za wanawake na kuboresha miundombinu ya utunzaji wa watoto.
Takwimu za hivi karibuni za sensa zilionesha kupungua kwa kasi ya kiwango cha kuzaliana.
No comments