Azam FC yamnasa mshambuliaji Idris Mbombo kutoka El Gounah ya Misri
KLABU ya Azam FC imemsainisha mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, kutoka El Gounah ya Misri.
Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu yetu hadi mwaka 2023.
Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors, zote za Zambia, anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita ililtegemea zaidi Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo.
Huyu anakuwa mchezaji mpya wa sita dirisha hili kubwa la usajili baada ya Mkenya, Kenneth Muguna, Wazambia watatu, Charles Zulu, Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.
No comments