WHO yatoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya China
Shirika la afya ulimwenguni WHO limeidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya Covid-19 iliyotengezwa na kampuni ya China ya Sinopharm.
Uamuzi huo utawezesha mamilioni ya dozi kuweza kuzifikia nchi zenye uhitaji kupitia mpango wa kimataifa wa usambazaji chanjo.
Timu ya washauri wa WHO, imesema hatua hiyo inafungua uwezekano wa chanjo ya Sinopharm kujumuishwa katika mpango wa COVAX katika wiki chache zijazo na kusambazwa kupitia ofisi za kanda za WHO na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhahom Ghebreysus amesema hatua hiyo inaongeza orodha ya chanjo ambazo COVAX inaweza kuzinunua na kuzipa nchi ujasiri katika kuagiza na kusimamia chanjo.
Chanjo ya Sinopharm imetengenezwa na taasisi mbili za kibaiolojia za mjini Beijing na Wuhan.
No comments