Header Ads

Header ADS

Mwanaume Amdai Mkewe Figo yake Aliyompa Baada ya Kuachana


Raia wa Marekani Richard Batista alitoa figo moja June 18, 2001 na kumpa Mkewe Dawnell Batista baada ya figo mbili za Mke huyo kufeli, baadaye mwaka 2009 baada ya Mwanamke huyo kudai talaka ili waachane, Richard akafungua kesi Mahakamani akidai arudishwe figo yake au alipwe USD Mil 1.5.


Mahakama ilitoa maamuzi ya kwamba figo haiwezi kurudi (sio sehemu ya mali za kugawana Watu wakiachana) na Mwanamke hawezi kulipa pesa kwakuwa kuchangia figo ni kama zawadi ambayo thamani yake hakuna Pesa ya kuinunua na pia kudai figo ni sawa na kutaka kumuua anayedaiwa.



No comments

Powered by Blogger.