Header Ads

Header ADS

Shirika la Posta Tanzania Sasa Kidigitali Zaidi






SHIRIKA la Posta Tanzania limejidhatiti kuboresha huduma zake kidigitali kuendana na mabadiliko makubwa ya teknolojia kote duniani ili kurahisisha huduma zake kwa wateja na kutanua wigo wa soko la huduma hizo.

 

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Aprili 23, 2021, na uongozi wa Shirika hilo chini ya wizara ya teknolojia ya mawasiliano wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari katika makao makuu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.

 



 

Akizungumza katika mkutano huo, Jason Kalile ambaye ni mwakilishi wa Posta Mkuu Tanzania amesema; “Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, Shirika la Posta nchini limekusudia kuboresha huduma zake kuendana na mabadiliko ya teknolojia na vionjo vya wateja.

 

“Ili kutimiza hayo,hivi karibuni shirika letu linaimarisha mifumo ya kiteknolojia ili kuendana na wakati ambapo hivi karibuni huduma mpya ya posta kiganjani itazinduliwa nah ii tunaamini itarahisisha sana huduma zetu.

 

Aidha, Shirika la Posta Tanzania ambalo ni mjumbe wa Tanzania Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta Dniani (kwa kuchaguliwa miongoni mwa nchi 40 washirika) kwa sasa linashiriki mkutano wa kimataifa wa wananchama wa Umoja huo ambapo mkutano huo unafanyika kwa njia ya online kutokana na janga la covid 19 duniani kote.

 



 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano (Zainab Chaula) mwakilishi wake, Injinia Clalence Tukeleza ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, amesema;

“Kuna mikutano mbalimbali inayoendelea kwa sasa kuanzia mkutano mkuu wa Umoja wa Posta Duniani unaoshirikisha Mawaziri kutoka nchi wananchama.

 

“Tanzania ni mjumbe wa Baraza la Uendeshaji la Umoja huo lililoanzishwa mwaka 1874, kwa sasa tunashiriki mkutano wa Baraza hilo ambao hufanyika mara mbili kwa mwaka. Aidha kuanzia Jumatatu tutashiriki katika mkutano wa Baraza la Utalawa ambapo Tanzania ni mjumbe mwalikwa.

 



 

“Mkutano huu unaangazia masuala mbalimbali yakiwemo ya uendeshaji, ubora wa huduma. Umoja huu umetusaidia kuboresha na kukuza sekta yetu ya mawasiliano hususani posta, kutuma na kupokea vifurushi na kukuza mashirikiano yetu nan chi nyingine. Tunatumia nafasi yetu kuwakilisha nchi yetu vzuri kutetea maslahi ya wananchi wetu katika masuala ya posta.

 

“Aidha, Tanzania kupitia Shirika la Posta inasimamia kituo cha kutekeleza teknolojia kwa nchi zote za Afrika zinazozungumza lugha ya Kingereza na Msumbuiji. Wizra ya teknolojia ya Mawasiliano imeendelea kuboresha teknolojia ya posta na sera pia iendane na mabadiliko ya teknlojia kuendana na mahitaji hivyo kuchagia ukuaji wa uchumi wa uchumi wa kidigitali.

 

 

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Emmanuel Manase amesema TCRA kupitia Shirika la Posta, wanayo majukumu kadhaa ambayo ni pamoja na kuishauri serikali kuhusu masuala ya posta ikiwemo sera na kanuni, kutoa leseni za uendeshaji, kusimamia utoaji wa huduma za posta, kuiwakilisha Tanzania kimataifa kuhusu masuala ya posta pamoja na kusimamia viwango vya ubora vya usafirishaji.

 



 

Aidha, ameongeza pia kuwa, ili kuboresha huduma hizo kiteknolojia, kwa sasa wanaendelea kufufua mfumo wa kiteknolojia upimaji wa huduma Global Monitoring System kwa ajili ya huduma za ubora. Kutekeleza mpango wa anuani za makazi na kuendeleza miundombinu ya posta.

 

Shirika la Posta ambalo leseni yake iliisha 2019, imepewa leseni mpya itakayokwenda mpaka mwaka 2043 ambapo imeelezwa kuwa manufaa ya kujiunga na Umoja wa Posta duniani ni kutanua wigo wa kuhudumia nchi zote wanachama.

 

“Ukijiunga unakuwa wakala wa mashirika yote ambayo yamejiunga dunia nzima, utatoa huduma ya mizigo na vifurushi (kutuma au kupokea) kutoka nchi hizo au wananchi wa Tanzania. Posta ni zaidi ya barua, unaweza pia kutumia huduma za kibenki kutoka nchi mbalimbali,” amesema Mwakilishi wa Mkuu wa Posta.

 


No comments

Powered by Blogger.