Mondi Nyuma Ya Rayvanny, Harmonize
Wakati sheria ikisubiriwa kuchukua mkondo wake juu ya kusambaa kwa picha na video za utupu zinazodaiwa kuwa za staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, kwa upande wa bosi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaona ni freshi tu.
Habari za ndani zinadai kwamba, tangu mwanzo, Diamond au Mondi alikuwa nyuma ya sakati hilo lililomhusisha msanii wake mwingine, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ dhidi ya Harmonize au Harmo.
HAKUTAKA KUWA MSTARI WA MBELE
Chanzo hicho kimeeleza kwamba, mwanzo wa sakata hilo, Mondi hakutaka kuwa mstari wa mbele, lakini alikuwa anaunga mkono ushindani unaojengeka kati ya Harmonize ambaye aliondoka kwenye lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) na kwenda kuanzisha ya kwake ya Konde Gang Music Worldwide na Rayvanny ambaye naye ameanzisha lebo yake ya Next Level Music.
Inasemekana kwamba, Harmonize na Rayvanny wamekuwa na uhasama huo ili kukuza muziki wao, jambo ambalo linapata baraka zote kutoka kwa Mondi.
“Kiki ndizo zilizomkuza na Diamond kwa hiyo anajua umuhimu wake. Anajua ni kwa jinsi gani zinamfanya mtu anakuwa midomoni mwa watu.“Harmonize na Rayvanny ni wanafunzi wazuri wa Diamond na wanaonekana kweli wamefuzu.
“Lakini mashabiki wanapaswa kukumbuka kwamba, wakati sakata hili la Harmonize na Rayvanny linaibuka, kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wanamlinganisha Diamond na Harmonize, jambo ambalo Diamond hakulitaka kabisa.
ATAKA KUBAKI NA KIBA
“Aliona kulinganishwa na Harmonize ni kushushwa, alitaka kubaki na ule ushindani wake na King Kiba tu,” anasema mtu wa karibu wa mastaa hao.
MONDI ANAONA FURSA
Katika kuonesha kwamba anafurahishwa na sakata hilo na anaona lina faida kubwa kuliko hasara na bila kujali kuna masuala ya kisheria, katika maoni yake, Mondi anaona ni fursa kwao kwa ajili ya kushindanisha kazi zao kuona kama ni nani mwenye mafanikio zaidi kati yao.
Mondi anasema kuwa, haona kama ni sawa kupelekana Polisi huku akikanusha kwamba siyo kitu ambacho aliwafundisha kama baadhi ya watu wanavyosema kwenye mitandao ya kijamii.“Wasiwe wanapelekana Polisi, mara nini, siyo kitu ambacho labda niliwafundisha.“
Hata ukitazama hata kwetu sisi kaka zao kama mimi na Ali Kiba, hajawahisi kusikia kuna siku tumepelekana Polisi au mahakamani.“Tunakuwa tunashindana tu kwenye masuala ya kazi au nini,” anasema Mondi.
WASHINDANE KWA WAFUASIA
nasema kuwa, ni vizuri wakashindana kwa kuwa na views (watazamaji) na wafuasi wengi na siyo mambo ya kupelekana Polisi.Wakati wote wa sakata la Rayvanny na Harmonize, Diamond hakusikika popote, lakini ametoa kauli hiyo wakati ishu zimeumana kwani tayari watu kama Rayvanny, Kajala, Paula, Baba Levo, Juma Lokole na wengine wamefikishwa Polisi kwa madai ya kusambaza video chafu iliyodaiwa ni ya Harmonize.
PROFESSOR JAY: UHASAMA UMEVUKA MIPAKA
Akizungumzia bifu hilo la Harmonize na Rayvanny, Mkongwe wa Muziki nchini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay alisema licha ya kwamba Harmonize ni kijana anayejituma lakini anashauri washindane kwenye kazi kwa sababu uhasama wao umevuka mipaka.
Akizungumza katika kipindi cha Bongo 255 cha 255 Global Radio Professor Jay alisema, “naona kama imevuka pale inaenda person na hii inaleta uhasama.
“Haya mambo tukishaanza kushabikia mambo ya timu kuna siku Harmonize na Rayvanny watakutana uso kwa uso halafu mambo yatakuwa mabaya zaidi. Hatuko tayari kuona msanii yeyote anapotea ama kuona vipaji hivi vinapotea. Hakuna mtu akafanya bifu ikamsaidia.
“Niwaombe mashabiki na wasanii turudi kwenye mstari, tusapoti kazi zao ili iweze kuendelea lakini tusisapoti uchafu unaofanyika,“ alisema.
STORI: KHADIJA BAKARI, DAR
OPEN IN BROWSER
No comments