Meya adakwa na TAKUKURU arejesha fedha
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro imerejesha shilingi milioni 150 zilizokwapuliwa na Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu katika Benki ya Ushirika ya KCBL mkoani humo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu na kubainisha kuwa ndani ya kipindi hicho wamefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni 200.
"Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro tumefanikiwa kuokoa shilingi milioni 229,675,166 na kati ya fedha hizo watu ambao wamenufaika na fedha za KCBL visivyo halali ni Juma Raibu, Meya wa Manispaa ya Moshi ambapo amerejesha shilingi 150 milioni,” amesema Wikesi
Amebainisha kuwa fedha hizo zimerejeshwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na TAKUKURU baada ya uchunguzi kufanyika.
"Alichukua fedha hizo KCBL kabla benki hiyo haijaanza kuingia kwenye misukosuko ya kufilisiwa na sasa hivi tunaendelea kuchunguza watu wote walionufaika na fedha za benki hiyo na salama yao ni kuzirejesha fedha zote," ameongeza Wikesi.
No comments