Header Ads

Header ADS

Je Wajua Adolf Hitler Alikuwa na Korodani Moja?...Yafuatayo ni mambo usiyoyajua kuhusu Adolf Hitler



Nani ambaye hamjui Dikteta Adolf Hitler? Adolf Hitler ni mtawala maarufu zaidi katika karne ya ishirini, kiongozi wa chama cha Kinazi aliyeitawala ujeruman kati ya mwaka 1934 mpaka 1945. Kama ulikuwa hujui, hitler ndiye mwanzilishi mkuu wa vita ya pili ya dunia.

Yafuatayo ni mambo  usiyoyajua kuhusu Adolf Hitler.

Alipendelea zaidi kuangalia Filamu za mauaji, wafuasi wake walipenda kurekodi video pale walipokuwa wanawauwa wafungwa na kumpelekea Hitler!

Adolf Hitler Ndiye aliyeanzisha sheria ya kutovuta sigara hadharani. Alikuwa mvuta sigara enzi za ujana wake na alikuja kuacha baadae akidai ni utumiaji mbaya wa fedha.

Licha ya kufurahia Kuua sana binadamu, adolf alipinga sana ukatili wa wanyama, na alikuwa hali nyama ya aina yeyote ile.

Hitler aliokolewa kufa maji na mfanyakazi wa kanisa alipokuwa na umri wa miaka minne (4), na kwa kipindi hicho, hitler ilipenda saana awe mfanyakazi wa kanisa akiwa mkubwa.

Mpenzi wa kwanza wa Hitler alikuwa myahudi na aliona aibu kumueleza hisia zake. Baadae aligeuka na kuamua kuua kila myahudi aliyekuwepo ujerumani, kasoro daktari mmoja ambaye alisaidia bure familia ya hitler kuwatibu kutokana na ugumu wa maisha kipindi adolf akiwa mdogo.
Akiwa jela, Hitler aliwahi kuandika barua kwenda kampuni ya mercedes benz akiomba mkopo wa gari.

Alishawahi kushindania tuzo ya nobel mwaka 1939.

Alikuwa na Korodani Moja Baada ya Moja Kukatwa kutokana na kujeruhiwa vitani

Hakuwa anajua kuendesha gari mpaka alipokufa

Hakumaliza High School aliachia njiani

Hakupenda aina yoyote ya michezo licha ya kupenda kutolea mifano ya kabumbu katika hotuba zake.
Adolf Hitler alikuwa na baadhi ya tabia za kike akiwa na umri mdogo, alikuwa pia na mwandiko wa kike. Vilevile hitler alipenda sana chokoleti kiliko vyakula vyote!

No comments

Powered by Blogger.