Header Ads

Header ADS

Je, Unaifahamu Dawa ya Usingizi inayotumiwa na Wezi Kuwapulizia Watu Kabla ya Kuiba?


Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa CHLOROFORM.

Dawa hiyo ina uwezo wa kumlegeza au kumzimisha mtu kiasi kwamba ashindwe kujitambua na kuhisi chochote na wahalifu wakafanya chochote wanachoweza kwa muda wa kutosha. Wataalamu wa afya huitumia katika shughuli za kitabibu hasa wakati wa upasuaji.

 Madhara ya Chloroform kwa binadamu huongezeka sambamba na kiwango cha dozi yake. Wakati kiwango kidogo kinasababisha kutojielewa, kadri dozi inavyoongezeka huweza kukufanya uzimie kabisa au usisikie mguso wowote. Kwa kiwango kikubwa zaidi huweza kusababisha upumuaji wa shida, misuli ya mwili kutulia kabisa, misuli ya kifua kupooza na mwishowe kupelekea kifo.

Inahitajika tahadhari kubwa hasa kwa wasambazaji wa dawa hii ambayo imekuwa ikileta hasara kwa mali za watu kuibiwa katika nyumba zao nyakati za usiku.

No comments

Powered by Blogger.