Mume wa Queen Darleen atoboa siri hii kuhusu mke wake mkubwa
Isihack ambaye ni mume wa msanii Queen Darleen, ametoboa siri kwamba mke wake mkubwa anayetambulika kwa jina la #Sabra ni mjamzito na mimba ni yake.
Sabra ambaye ni mke mkubwa wa mume wa msanii huyo, wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita sasa lakini hawakuwahi kubahatika kupata mtoto.
Hata hivyo wakati mitandaoni kukiwa na taarifa kuwa mwanamke huyo amebeba mimba ya mwanaume mwingine na tayari ameshamtwanga talaka.
Akizungumza leo Jumanne Februari 9, 2021 katika kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, aliondoa utata huo na kueleza kuwa ni kweli #Sabra ana mimba na mimba ni yake wake.
Akijibu kwa kifupi swlai hilo amesema, "Ni kweli Sabra ni mjamzito na mimba ni yangu” amesema Isihack.
Kuhusu tetesi za kuachana na bimkubwa zinazoelezwa mitandaoni, #Isihaka alikanusha na kueleza kuwa ni mwanamke ambaye hatarajii kumuacha leo wala kesho kwa kuwa wametoka naye mbali na anajua thamani yake.
No comments