Mkwanja Anaolipwa Kocha wa Yanga Kaze, Makazi Yake Sio Poa
WAKATI Yanga ikiwa inaongoza ligi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze amekuwa akitumia kiasi cha shilingi milioni nane kwa siku 30 kulipa kodi katika nyumba anayoishi na familia yake.
Kaze amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Canada akitoka katika Akademi ya Barcelona ambapo ameiwezesha timu hiyo mpaka sasa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi huku wakiongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 35.
Kaze anayekunja mshahara wa dola 10,000 (Sh mil 23), analipiwa dola 120 (Sh 277,801) kwa ajili ya kulala tu.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimesema kuwa, kocha huyo yeye ameamua kuishi kwenye apartment akiwa na familia yake ambapo kwa siku analipia dola 120 kwa ajili ya kulala pekee pale Palm Village Mikocheni jijini Dar karibu na mabosi wa Azam FC.
“Mwalimu yeye anaishi katika apartment ya Palm Village kwa sababu yupo na familia yake hapa nchini, kwa upande wa bei yake pale imechangamka kidogo.
"Pale halipii yeye bali uongozi ndiyo unalipia, kwa siku moja wanasema ni dola 120 ingawa tofauti huwa wanalipa kwa bili ya mwezi ambayo inafika milioni nane kwa kuwa familia yake bado inaishi pale licha ya mwalimu mwenyewe muda mwingi kuwa Avic Town inapokuwa timu wakati wote,” amesema mtoa taarifa.
No comments