Haji Manara 'Tumekuja Kusaka Heshima Congo'
HAJI Manara, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba amesema kuwa kila kitu kuhusu maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya AS Vita kipo sawa wanaingia uwanjani kusaka heshima.
Simba itamenyana na AS Vita ya Congo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi unaotarajiwa kuchezwa Februari 12.
Jana, Februari 10 kikosi kimewasili Congo na kuanza kufanya mazoezi ambapo Joash Onyango ambaye alikuwa anaibukia majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe alikuwa miongoni mwa walioanza mazoezi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Manara amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wataingia kea nidhamu pamoja na kusaka heshima.
"Tunatambua kwamba tunawakilisha nchi na mashindano haya ni makubwa hivyo tutapambana kusaka heshima pamoja na ushindi ndani ya uwanja.
"Wachezaji na benchi la ufundi lipo sawa kwa Watanzania kikubwa
No comments