Boateng aondolewa katika kikosi cha Bayern, baada ya kufiwa na Ex wake
Saa chache baada ya taarifa kutoka mwanamitindo na mpenzi (Kasia Lenhardt) wa zamani wa staa wa FC Bayern Jerome Boateng kuwa amefariki Dunia jana ikiwa ni wiki moja baada ya kuachana, Boateng amejiondoa katika kikosi cha Bayern nchini Qatar.
Boateng ataukosa mchezo wa fainali ya Club Bingwa Dunia kati ya FC Bayern dhidi ya Tigres UANL ya Mexico ambapo utachezwa kesho nchini Qatar.
Kasia (25) alikutwa amefariki usiku wa Jumanne katika apartment yake Mjini Berlin nchini Ujerumani.
No comments