Babu Tale: Kuanzia Leo Mimi ni Chawa wa Magufuli
MBUNGE wa Morogoro Kusini-Mashariki, Hamisi Taletale maarufu kama Babu Tale, amesema kuwa kuanzia leo yeye amekuwa ‘chawa’ wa Rais John Magufuli kwa kuyasema mazuri yote ambayo rais amelitendea taifa hili.
Tale amesema hayo leo Ijumaa, Feebruari 12, 2021, wakati Magufuli akizindua kiwanda cha kusindika mazao ya kunde mjini Morogoro.
“Rais Magufuli, mimi ni mmoja kati ya watu wanaotembea kifua mbele nikiona maajabu yako kwangu, kwa sababu umenitoa chini na kuniweka juu na kunipa heshima. Hizi zote ni nguvu zako kupitia CCM, mimi kuanzia leo ni chawa wa John Pombe Magufuli,” alisema Babu Tale.
No comments