Tom Cruise Kuwa Mwigizaji wa Kwanza Kuingiza Akiwa Nje ya Dunia
Urusi inashindana na Marekani kuweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza kupeleka mwigizaji kufanya filamu Nje ya Dunia 'Space' baada ya Mmarekani Tom Cruise Kuungana na shirika la Safari za Anga la NASA na kampuni ya utengenezaji wa vyombo vya anga ya Elon Musk 'SpaceX' ili kumfanya kuwa mwigizaji wa kwanza kufanya filamu ya Action nje ya Dunia katika Kituo cha Anga cha Kimataifa 'ISS'. Filamu hio itagharimu zaidi ya US dola milioni 200 na itaanza kufanywa nje ya Dunia October 2021.
Urusi wameanza kusajili mwigizaji wa Kike, Sio lazima akidhi vigezo vyote vya uigizaji ila awe ni raia wa Urusi tu, umri wa miaka 25 hadi 40, awe na afya bora, uzito kati ya kilo 50 na 70, uwezo wa kukimbia km 1 kwa dakika tatu na nusu au chini na ajue kuogelea.
No comments