Papa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Afunguka Kuhusu Chanzo ya Corona...
Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, ametoa ombi kwa mamlaka duniani kuhakikisha chanjo ya COVID-19, zinapatikana kwa wote.Amesisitiza kuwa watu wanaopaswa kupewa kipaumbele ni wale walioko katika hatari na wasiojiweza, bila kujali ni nani ana hakimiliki ya chanjo hizo.Papa Francis amefananisha chanjo hizo kama “nuru ya matumaini” kwa ulimwengu.
Ameongeza kwamba ''hatuwezi kuruhusu ubinafsi wa kitaifa kuwa kisiki kutuzuia kuishi kama wanadamu kamili.''Ametoa wito kwa viongozi wa dunia, viongozi wa biashara na wa mashirika ya kimataifa kukuza ushirikiano badala ya ushindani, na watafute suluhisho kwa wote.Papa Francis pia aligusia masaibu ya watoto waliopo katika mazingira ya vita akitaja Syria, Yemen na Iraq.Amesema masaibu ya watoto hao yanapaswa kugusa nyoyo za watu wenye nia njema ili machafuko yapatiwe ufumbuzi, na juhudi zifanywe kujenga mustakabali wenye amani.
No comments