"Ni Wake Wenza 100 au Mpenzi Mtazamaji" - Lulu Michael Afunguka
Staa wa filamu Elizabeth Michael ni mmoja kati ya wasanii ambao wanajibu sana 'comments' za mashabiki wake pale wanapo-comment kwenye picha au video anazp-post kwenye mitandao ya kijamii.
Hilo limeendelea siku ya leo baada ya ku-post picha kwenye Instagram kisha mashabiki zake ku-comment kwenye picha hiyo, ila majibu aliyoyatoa yana ukakasi na kufanya watu kujiuliza ni picha au kuna kingine.
Shabiki wa kwanza ali-comment kuwa "Hivi ni nani alikuambia ukibadilisha rangi ya nguo hautapendeza maana kila siku ni gauni jekundu"
Elizabeth Michael alimjibu shabiki huyo kwa kuandika "Kuna hela yako yoyote unachangia inakuuma labda tulia kama mpenzi mtazamaji bro, nikusaidie tu nyekundu ni rangi yangu pendwa"
Shabiki alimchokoza kwa ku-comment kuwa "Umeona shepu mpya mjini ya mke mwenzio"
Aidha msanii huyo hakumuacha salama alimrudia kwa kumjibu "Nina wake wenza kama 100 hivi, sasa sijajua ni yupi"
No comments