Hatimaye Chidi Benz aichia video yake na 2Pac
Hatimaye msanii wa HipHop Chidi Benz ameachia ule wimbo wake 'Dont Cry' ambao alisema amefanya na mkali wa HipHop duniani 2Pac Shakur ambaye amefariki dunia kwa kupigwa risasi 1996.
Chidi Benz ameachia wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube na baadhi ya vipande vya video fupi ambavyo amevi-post kwenye ukurasa wake wa Instagram.
"Habari zenu kwa mara kwanza naangalia watu wanasemaje kuhusu kazi, naona watu 106 wamekubali na mtu mmoja hajakubali, kitu kikubwa maisha yote nashukuru Mungu kwa kufanikisha na kujiona mtu wa watu" ameandika Chidi Benz
Chidi Benz ni mmoja wa wasanii wa HipHop ambao wanakubalika sana hapa nchini na tayari ameshafanya kazi nyingi zilizofanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.
No comments