Wanachama Wasimba Wakata Mzizi wa Fitina, Wasema Liwalo na Liwe Mohamed Dewj (MO) Ndio Baba Lao
Hayo yameelezwa na Mhazi Mstaafu wa tawi hilo Fahimu Lardhi, alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa, ambapo alielezea masikitiko yake kutokana na kusakamwa kwa Mdhamini wao Mkuu Mohamed Dewj (MO), kitendo kilichofanywa na watu wasioitakia mema klabu hiyo.
Alisema kwamba kwa muda mrefu kuna baadhi ya watu wasioitakia mema Simba wamekuwa wakitumia mitandao ya Kijamii, kuhoji mikataba iliyowekwa kati ya MO na klabu hiyo hususani wakitaka kujua kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 20 zilivyotoka.
“Niwaombe wana-Simba wenzangu tusiwe wanyonge kiasi hiki, hivi sasa tuna miaka minne tumekuwa na utulivu wa hali ya juu, hii inatokana na Mdhamini wetu Mohamed Dewj kuiweka klabu katika misingi imara, ambayo wapinzani hawapendi,” alisema Lardhi.
Aliongeza kwa sema kuwa wapinzani wao Yanga hivi karibuni walitoa tamko zito kwa uongozi wao, wakiutaka umsimamishe mara moja aliyekuwa Kaimu Katibu wao kwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa, uongozi ukachukua hatua mara moja.
“Inakuwaje wenzetu Yanga wanachama wanathubutu kutoa tamko kwa viongozi wao tena la masaa lilitekelezwa na viongozi wao, sisi Simba tunashindwa nini kuwakemea wanaomsakama mfadhili wetu kwa lengo la kutaka kuihujumu klabu yetu,” alihoji Lardhi.
Mwisho Mhazini hiyo mstaafu alimalizia kwa kuwaomba wana-Simba katika matawi kuongeza umoja, upendo na mshikamano kwa viongozi ili timu yao iendelee kufanya vema kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
“Viongozi tuliowapatia dhamana ya kuiongiza klabu wapo wachache, ni jukumu letu sisi viongozi wa matawi, wanachama, wapenzi na mashabiki kwa umoja wetu tuwapatie ushirikiano mkubwa ili waweze kufanikisha malengo yetu,” alimalizia Lardhi.
No comments