Header Ads

Header ADS

Jezi ya Marehemu Maradona Yampoza Messi, Barcelona Yapigwa Faini ya Mamilioni Kisa Jezi Hiyo




Klabu ya Barcelona italazimika kulipa faini ya paundi 2,700 baada ya nyota wake Lionel Messi kuvaa fulana yenye ‘brand’ ya Adidas katika kutoa heshima zake kwa gwiji wa soka Diego Maradona baada ya kufunga goli dakika ya 73 kwenye mchezo wao dhidi ya Osasuna siku ya Jumapili.

Barcelona will have to pay a £2,700 fine after Lionel Messi paid tribute to Diego Maradona

Messi alivua jezi ya Barcelona ambayo mdhamini wao mkuu ni Nike na kubakiwa na jezi ya klabu ya Newell’s Old Boys yenye ‘brand’ ya Adidas timu ambayo Maradona aliitumikia mwishoni mwa zama zake za kucheza mchezo wa soka.

Maradona, who died last week at the age of 60, played for Newell's at the end of his career

Moja kati ya vitendo ambavyo Messi amevifanya baada ya goli hilo ni pamoja na kubusu mikono yake yote miwili na kutazama juu kama vile Maradon alivyokuwa akifanya enzi za uhai wake katika kusakata kabumbu.

Lakini kitendo hicho kimekuwa kinyume na kanuni za Royal Spanish Football Federation ambao kwa sasa wapo tayari kuipiga faini klabu hiyo kutokana na kitendo hicho cha Messi.

Baada ya mchezo huo Messi aliposti picha yake akiambatanisha na picha ya zamani ya Maradona wakiwa katika aina moja ya ushangiliaji.

Messi aliwahi pia kuichezea klabu ya Newell’s Old Boys kabla ya kujiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13. Maradona kwa upande wake alipata kuichezea michezo mitano Newell’s mwishoni mwa zama zake za soka.



No comments

Powered by Blogger.