Tory Lanez Akana Mashtaka ya Kumshambulia kwa Risasi Rapa Megan Thee Stallion
Tory Lanez amekana mashtaka ya kumshambulia kwa risasi rapa Megan Thee Stallion mwezi Julai mwaka huu.
Kwenye muendelezo wa kesi hiyo jana mahakamani ambapo mwanasheria wa Tory Lanez Bwana Shawn Holley alihudhuria kwa niaba, alikana mashtaka hayo na kusema mteja wake hana hatia kwenye mashtaka yote mawili ya jinai; Kushambulia na pia kubeba silaha yenye risasi.
No comments