Simba Watoa Ushirikiano Upangaji Matokeo
KLABU ya Simba imewaombwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka za dola katika uchunguzi unaoendelea kufanywa na mamlaka hizo kuhusu tuhuma za upangaji matokeo.
Hivi karibuni aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama wa Simba, Hashim Mbaga alikamatwa na Polisi akituhumiwa kuihujumu klabu hiyo na mapema wiki hii aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa naye aliitwa kuhojiwa ikidaiwa ni mahojiano ya tuhuma hizo za upangaji matokeo.
"Wakati tukiwa tunaendelea kusubiri matokeo ya uchunguzi huo, tunasikitishwa na kubainika kwa njama za upangaji matokeo na kuihujumu Simba,"
"Tunalaani vitendo na njama zozote ya kupata motokeo ya mpira nje ya uwanja, klabu ya Simba tunajivunia rekodi yetu uadilifu katika soka.
"Tunaimani kwamba uchunguzi unaondelea utapelekea hatua thabiti za kuthibiti tabia chafu ya kupanga matokeo tabia inayo haribu sifa na hadhi ya soka.
"Tunaviomba vyombo vya uendeshaji soka nchini navyo vianze uchunguzi kuhusu suala hili na kuchukua hatua kali ili kukomesha tabia hii," alieleza taarifa hiyo
No comments