Header Ads

Header ADS

Mobeto Aambiwa ana Damu ya Kunguni



MWANAMAMA ambaye ni mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ameambiwa kuwa siyo siri ana damu ya kunguni.


Hii ni baada ya Mobeto ambaye ni baby mama wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuposti video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa anawafundisha watoto wake ambapo tofauti na matarajio ya wengi kwamba alistahili pongezi, mambo yalikuwa kinyume kwani alipokea makavu laivu kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake


Baadhi ya mashabiki hao walisema kwamba ana msongo wa mawazo ndiyo maana ameamua kuwafundisha watoto na kama hatakuwa makini, basi anaweza kujikuta hospitalini kwa matatizo ya afya ya akili.


 


Imedaiwa kwamba, tangu mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye naye ni baby mama wa Diamond awasili Bongo, Mobeto amekuwa akitupiwa vijembe ambavyo vinaaminika kwamba huwenda vinamchanganya.


 


“Stresi ni mbaya ninyi mpaka ameamua kuwa mwalimu wa chekechea wa kujitolea ili tu apunguze mawazo. “Tukunyema ajaribu kukaa hivyo, kama hatalazwa hospitalini mwezi mzima….Povu ruksaaa… “Stresi hizi jamani, yaani unaweza kujikuta yaya bila kupenda… “Drama tu…tangu lini mambo hayo ya kumfundisha mwanao nyumbani?


 


Kwani shuleni walimu wamekwenda wapi,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki ya kumponda. Hata hivyo, akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA juu ya kusemwa vibaya na kwamba ana damu ya kunguni, Mobeto alikuwa na haya ya kusema; “Nimewazoea na wala hawanikeri hata kidogo…”




No comments

Powered by Blogger.