Madhara ya Kubana Mkojo Kwa Muda Mrefu
Watu wengi huvumilia mkojo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi wanaweza wakawa katika eneo ambalo hawezi kwenda haja ndogo lakini wengine ni uzembe ambapo wengi utakuta anaangalia tamthilia hivyo hataki apitwe, au anaona akienda haja ndogo hadi arudi umbea unaopigwa utampita na hivyo anaamua kubana mkojo, hayo yote yana madhara kwa mwili wako.
Je! Wewe hukojoa mara ngapi kwa siku? Mbili?, Tatu? Tano? Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali, wamesema kuwa kila mtu anatakiwa kukojoa kila baada ya saa 4 hadi 6, lakini kama utashikilia mkojo wako kwa muda zaidi, utakuwa uanajiweka kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo mbalimbali.
Haya ni baadhi ya madhara yatakayokupata endapo utabana mkojo kwa muda mrefu zaidi;
1. Kujikojolea
Kwa mujibu wa Daktari Lauren Streicher akifafanunua hili alisema kwamba, mtu anapaswa kufikiria kibofu chake kama puto ambalo limejazwa maji kupitiliza. Puto hilo likatanuka hadi mwisho wake na kuwa zito, kadiri utakavyokuwa unazidi kuubana, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwako wewe kutembea hadi chooni kabla hujajikojolea.
Itakuwa ni aibu kwa mwanamke mtu mzima kujikojolea eti kwa sababu hakwenda chooni kwa kunogewa na muvi au umbea ambapo pengine hauna faida.
2. Kulegea kwa misuli ya Pelvic
Misuli ya Pelvic hutumika katika kuzuia mkojo usitokea au kuuruhusu utoke katika kibofu cha mkono. Ukiwa na tabia ya kubana mkono kwa muda mrefu sana, misuli hii itachoka na hivyo kuacha kufanyakazi kwa usahihi. Hilo linapotokea unashindwa kuzuia tena mkojo wako sababu misuli imelegea na hivyo mkojo ukija unapita moja kwa moja.
Hivyo, epuka kuharibu misuli hiyo kwa kubana mkojo kwa vitu ambavyo sio vya msingi. Kila unapohisi mkojo nenda kakojoe kisha rudi, endelea na ulichokuwa unafanya.
3. Maumivu
Kwa kawaida unaposhikilia mkojo kwenye kibofu kwa muda mrefu, unapatwa na maumivu makali, lakini maumivu hayo hutokomea mara tu unapokwenda haja ndogo. Maumivu hayo yanaweza yakawa ni mfumo wako wa maisha kama hutachukua tahadhari mapema.
Waswahili husema kuwa, tabia hujenga mazoea, na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa misuli ya mwili wako, ukizoea kubana mkojo kila mara, itakua ikiima kila mara.
4. Kutanuka kibofu
Basi tusema kwamba ukibana mkojo kwa muda mrefu, kibofu chako kinaweza kisipasuke kutokana na wingi wa mkojo lakini kikatanuka kuliko ukubwa wake unaotakiwa.
Tatizo la kutanuka kwa kibofu kutokana na kubana mkojo mara kwa mara ni kwamba mwili wako utakuwa haukupi taarifa kuwa unatakiwa kwenda kujisaidia. Hii ni kwa sababu umbo la kibofu limeongezeka. Taarifa hizo ambazo hutolewa na ubongo wakati kibofu kimejaa ni muhimu sana, lakini kibofu kikitanuka hutozipata.
Ni kweli wakati mwingine unaweza ukabanwa na mkojo na kuwa sehemu ambayo huweza kupata msaada ya kujisaidia, lakini epuka tabia hii kuwa mazoea.
No comments