Kunani Tena.... Harmonize Ametangaza Kuahirishwa kwa Tamasha la Harmo Night Carnival
Mwimbaji Harmonize ametangaza kuahirishwa kwa tamasha la #HarmonightCarnival lililokuwa lifanyike kwa siku tatu kuanzia Novemba 28 mwaka huu. Akitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa tamko hilo, Harmonize hajaweka wazi sababu zilizopelekea tamasha hilo kuahirishwa.
Miezi minne iliyopita, Harmonize, Konde Gang wakishirikiana na E-FM & TV walitangaza uwepo wa tamasha hilo ambalo walisema lingejumuisha shughuli nyingi pia burudani ya muziki toka kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi.
No comments