Je Wajua Kuwa Mchezaji Simon Msuva Alikuwa Dancer wa THT? Mwenyewe Afunguka Ruge Kumshauri Acheze Mpira
Simon Msuva amemtaja marehemu Ruge Mutahaba kama mtu ambaye alimfanya aingie kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Winga huyo wa Taifa Stars na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco alikuwa ni mnenguaji (dancer) hodari akiwa Jumba la Vipaji Tanzania (THT) kipindi hicho, lakini baada ya marehemu Ruge kumuona siku moja akicheza mpira, alimuita ofisini na kumwambia aachane na unenguaji na ajikite kwenye soka
-
"Marehemu Boss Ruge ndiye alinishauri niingie kwenye mpira. Nilikuwa ninapenda Ku-Dance, akanifuata na kuniambia kuwa nina kipaji cha mpira. Akaniambia nitakuja kumkumbuka." alisema Simon Msuva.
No comments