Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Chahamishiwa Ofisi ya Rais ili Kuboresha Utendaji
Rais Magufuli amehamisha Kituo cha Uwekezaji #Tanzania (TIC) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ofisi ya Rais ili kuboresha utendaji kazi wa kituo hicho ikiwemo kupunguza urasimu kwa wawekezaji
Amesema anataka Mwekezaji mwenye fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14 hivyo amekihamisha ili wanaokwamisha akapambane nao yeye mwenyewe
Akiwa Bungeni Dodoma amesema, "Sekta binafsi itapewa umuhimu wa pekee sana. Watanzania ni matajiri lakini baadhi yao wanasita kuwekeza hapa nchini kwa kuogopa kusumbuliwa na maswali yasiyo na msingi. Tunahitaji mabilionea wengi wa Kitanzania"
Ameongeza “Tutapunguza foleni Barabarani, tutapanua Viwanja Vya Ndege 11, tutaboresha upatikanaji wa huduma za umeme, tutafikisha umeme kwenye vijiji vyote vilivyobaki.Upande wa Afya tutahakikisha Watanzania wote wanakuwa na Bima ya Afya na kuongeza Hospitali"
No comments