JE, Hujaona Siku Zako (Hedhi) na Huna Mimba? Majibu ya Hali Hiyo Yapo Hapa..!!!
Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakikosa la kufanya pale wanapoona siku zao za mzunguko (hedhi) zimefika halafu bado hawajaona siku hizo.
Hali hiyo huwapelekea wengi wao kuwa na maswali mengi, huku wengi wao wakianza kufikiri kuhusu ujauzito, lakini wanapopima ujauzito kwa bahati mbaya hukuta hakuna kitu hapo ndipo huzidi kuchanganyikiwa zaidi.
Sasa leo napenda tufahamishane hizi sababu ambazo huweza kuchangia siku zako kuchelewa kuonekana:-
1. Mabadiliko ya shughuli zako za kila siku
Huenda umeajiri sehemu mpya ambayo inakulazimu kubadili mfumo wako mzima wa maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na muda wa kuamka au umesafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hali hiyo na mengine huweza kuwa chanzo cha mabadiliko ya mzunguko wako ikiwa ni pamoja na kuchelewa.
2. Msongo wa mawazo 'stress'
Msongo wa mawazo ni mojawapo ya sababu ambazo huweza kuchangia kuvuruga mzunguko wako wa hedhi na kuchangia siku zako kuchelewa pia.
3. Magonjwa
Pale mwili unapopatwa na mabadiliko yakiwemo ya kuumwa nayo huweza kuwa sababu ya kubadili mzunguko wako wa hedhi na kuchangia pia kuchelewa kuona siku zako, kwahiyo ukiona hali hiyo unaweza kurudisha nyuma kumbukumbu zako na kukumbuka endapo wiki moja au mbili nyuma kama ulikuwa unaumwa au ulikuwa sawa.
4. Mabadiliko ya uzito.
Kuongezeka au kupungua kwa uzito huweza pia kuwa chanzo cha tatizo hili, hii ni kwasababu watu wenye uzito mkubwa au wenye uzito mdogo kunawakati huweza kujikuta wakiingia kwenye tatizo kama hili la kuchelewa kuona siku.
No comments