Header Ads

Header ADS

Hizi Hapa Picha Kali za Muonekano wa Stendi Mpya ya Mabasi Mbezi

 


Kutoka Mbezi Louis Dar Es Salaam, hii ni Drone Video ya Stand Mpya ya Kisasa ya Mabasi ya Mikoani iliyogharimu Tsh. Bilioni 71 ikiwa na uwezo wa kuruhusu Mabasi zaidi ya 1000 na Taxi 280 kupark, agizo la Rais Magufuli la Stand kukamilika kwa baraka limefanyiwa kazi na sasa kazi zinafanyika usiku na mchana.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Aboubakar Kunenge Ujenzi wa Stand hii umefikia 90% na itaanza majaribio ya Kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30 mwaka huu.


RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stand hii ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hotel ambapo zoezi la kutuma maombi limeanza November 09 hadi November 25.








No comments

Powered by Blogger.