Wafungwa Congo Wafa Kwa Njaa....Tunalishwa Kikombe Kimoja cha Uji Baada ya Masaa 72
Wafungwa katika Gereza la Bunia mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na baa la njaa, baada ya wawili kufafiki dunia wiki iliyopita kutokana na hali hiyo na kufanya idadi kufikia 17 tangu mwezi Aprili.
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, yanasema mamia ya wafungwa hupoteza maisha kila mwaka katika mazingira kama hayo.
"Hatuna chakula, hatuna dawa na hata pia mahali pa kulala. Tunapewa tu kikombe kimoja cha uji na hiyo baada ya masaa 72, " amesema mmoja wa wafungwa hao.
Kiongozi wa gereza la Bunia, Meja Camille Nzonzi, amesema hali hii inasababishwa na serikali.

No comments