Reginald Mengi alikuwa sio mtanzania wa kawaida, alikuwa ni mtu wa aina yake.
Navosema reginald mengi hakuwa mtanzania wa kawaida, sisemi ivo kwasababu ya utajiri au umaarufu wake..
Ni kwasababu aliweza ku-maintain utajiri wake na aliweza ku-maintain kuishi lifestyle ya kitajiri mbele ya jamii kwa miaka 25 mfululizo, tangu mwaka 1995 alivotoa tsh million 300 za skuvi na kufanya party za walemavu kila mwaka tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2019 aliofariki kama sikosei..
Alikuwa na ujasiri mkubwa sana wa kuonesha lifestyle yake hio ya kitajiri mbele ya jamii, bcoz wote tunavojua pesa na biashara ni vitu ambavyo havitabiriki, Leo unazo kesho huna, Leo unapanda gari yako binafsi kesho huna nauli ya daladala..ukiwa tajiri hlf ufilisike ni aibu kubwa.
Mnaweza mkaona ni rahisi, lakini Ku-maintain utajiri na lifestyle ya kitajiri alioishi reginald mengi mbele ya jamii kwa miaka 25 mfululizo sio mchezo, party za walemavu kila mwaka na michango + misaada ya mamilioni ya shilingi kila mwaka si mchezo sometimes alikuwa anatoa hadi msaada wa tsh billion 1..shida sio kupata utajiri au kuishi kitajiri, shida ni ku-maintain hiyo status, ukizingatia mzee mengi alitajirika tangu miaka ya 1984..
Ukitaka ujue ku-maintain utajiri, na lifestyle ya kitajiri ni vigumu, muulize mike tyson alielipwa USD million 400 (tsh billion 800 za kibongo) akaishia kufilisika, waulize asilimia 65% ya wacheza kikapu wa marekani, waliolipwa mabilioni ya shilingi lkn Leo wako juu ya mawe hata kuhudumia vizuri familia zao wanashindwa, hadi wanaaibika mbele ya jamii..
Ni hayo tu.
AlphaMale
No comments