Wachezaji hawawezi kucheza dk 90, hasa Watanzania – Kocha mpya Yanga, Zlatko Krmpotic
Kocha mpya wa klabu ya Yanga, Zlatko Krmpotic ametoa tathimini yake baada ya kuwashuhudia vijana wake wakitoka sare ya goli 1 – 1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21.
Zlatko Krmpotic amesema kuwa wachezaji wengi wa Yanga hawawezi kucheza dakika 90 na kutia mkazo hasa wachezaji Watanzania.
”Wachezaji wengi hawawezi kucheza dakika 90, hasa wachezaji hawa wa Tanzania. Wachezaji wa Tanzania hawawezi kucheza dakika 90. Lakini katika kipindi hiki tupopamoja tuta shirikiana katika kazi ili kuanza vizuri.” – Zlatko Krmpotic
Raia huyo wa Serbia ameongeza kuwa kuchelewa kujiunga na timu kwa wachezaji wakigeni nako kumechangia ”Kipindi cha kwanza tumeanza kwa kucheza vibaya sana sijui lakini ndiyo mpira. Nafikiri tulicheza vizuri katika kipindi cha pili lakini kucheza vizuri bila kufunga hakuna haja. Baadhi ya wachezaji wakigeni wamekuja kabla ya siku tatu, nne, tano.”
Akizungumzia mchezaji kutoka Angola, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo maarufu kama Carlinhos, kocha Zlatko Krmpotic amesema kuwa bado anahitaji muda ”Mchezaji Carlos kutoka Angola nadhani mchezaji huyu bado hajawa tayari kucheza dakika 90. Carlos (Carlinhos) ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji lakini anahitaji muda ili kuweza kucheza dakika 90.”
No comments