Mbaroni Akituhumiwa Kuchoma Moto Basi Lake
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu akiwemo mmiliki wa basi la kampuni ya HBD lenye namba za usajili T 321 DKW, Ahmedi Hemed (25), kwa tuhuma za kuchoma moto basi hilo na kusingizia kuwa moto huo ulitokana na matatizo ya mfumo wa breki
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa watuhumiwa hao walikula njama ya kufanya tukio hilo baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la basi hilo kwa moja ya taasisi za fedha nchini linalodaiwa kufikia zaidi ya sh. milioni 200.
No comments