Header Ads

Header ADS

Afrika Kusini yamkemea Trump kwa 'Kumdharua' Mandela



Chama tawala cha Afrika Kusini -South African National Congress (ANC) kimemuita rais wa Marekani Donald Trump kuwa mtu "anayesababisha uhasama, mwenye chuki dhidi ya wanawake na asiye na heshima " kilipokuwa kikijibu ripoti kwamba alimpuuzilia mbali Nelson Mandela , rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo.
Bwana Trump alisema kuwa mshindi wa tuzo ya amani "hakuwa kiongozi ", kwa mujibu wa wakili wake wa zamani Michael Cohen.

Madai hayo yanatoka katika kitabu kipya cha Cohen -Disloyal: Kitabu kinachoelezea maisha yake. Ikulu ya Marekani White House inasema kuwa Cohen ni muongo.

Kitabu chake pia kinasema kwamba Bwana Trump ana tabia kama za mjumbe wa kikundi kinachofanya ghasia za uhalifu na "anawadharau watu wote weusi "

Katika jibu lililojaa ukosoaji, chama cha ANC, ambacho Mandela alikiongoza kuanzia mwaka 1991 hadi 1997, kilisema kwamba "watu wote wanaopenda uhuru wa dunia wanasikitishwa sana na matusi haya ambayo yanatoka kwa mtu ambaye binafsi hana uwezo wa kuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa ".

"Trump ni mtu anayesababisha uhasama, anayewachukia wanawake na asiye na heshima kuwahi kuchukua wadhifa wa rais," iliongeza.

Kinyume chake, Mandela alisimama kama kiongozi aliyewaunganisha watu, ambaye "alifika katika maeneo mbali mbali ya dunia na kuleta amani na haki ya jamii ", ANC ilisema.



No comments

Powered by Blogger.