Header Ads

Header ADS

Siwezi Kukaa Benchi Kisa Mshahara''Kichuya''


Kiungo mshambuliaji wa Namungo Fc Shizza Kichuya amesema hajajiunga na timu hiyo kwa mkopo isipokuwa amesajiliwa na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Simba sc kumalizika.

Kichuya ameshindwa kuweka wazi mkataba wake na timu yake ya Namungo fc huku akishangazwa na taarifa zinasema yuko kwa mkopo katika timu hiyo yenye masikani yake mjini Ruangwa mkoani Lindi.

'' nilipomaliza mkabata wangu wa miezi sita na Simba, nlifatwa na timu nyingi lakini mimi na meneja wangu tukaona sehemu ya mimi kucheza na kurudisha ubora wangu ni Namungo na mimi naamini kupitia hii timu nitafanya vizuri hata kuliko Simba'' amesema Kichuya.

Aidha Kichuya amesema hawezi kuwapa ushauri wachezaji ambao wapo katika vilabu vya Simba na Yanga ambao hawapati nafasi katika timu hizo.

''Wachezaji wengi tunapofika katika timu za Simba na Yanga tunaona kama tumeridhika hata kama usipopata nafasi ya kucheza tunaona sawa kwa kuwa eti tunalipwa mishahara,ila kwangu naona sio sawa,ila kwa wengine ndiyo maana mimi siwezi kuongelea lolote kuhusu hilo'' amesema Kichuya.

Kikosi cha Namungo kinaratajia kuondoka Dar es salaam siku ya ijumaa tayari kabisa kwenda Arusha kwaajli ya mchezo wa Ngao jamii dhidi ya Simba utaopigwa siku ya jumapili hii .

No comments

Powered by Blogger.