Header Ads

Header ADS

Jux Adai Kama ingekuwa Hivi Agemkaribisha Vanessa



Mkali wa muziki wa RnB Bongo Jux amefunguka kusema ameandaa show ya kwa ajili ya watoto wa kike tu kwa sababu wamekuwa wakumuonyeshea upendo na sapoti iliyopitiliza.


Jux ameendelea kusema katika show hiyo hawaturuhusiwa wanaume kwa sababu haiwahusu, pia kwa sasa yupo single ila anaweza akapata mpenzi mpya siku hiyo ya tukio la show yake pamoja na wanawake.

Kama ilivyo ada huwezi ukamzungumzia Jux halafu usimtaje Vanessa Mdee, sasa wakati anazungumza hayo aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu uwezekano wa uwepo wa mpenzi wake huyo wa zamani.

"Kiukweli ningetamani uwepo wake maana nimewaambia watu wangu waalike wanawake wote ambao wapo kwenye hii Industry, naamini Vanessa Mdee ni mtu ambaye yupo kwenye Industry ila nilisikitishwa na taarifa zake za kuacha muziki japo sio kwa ubaya, pia naamini atakuwa hayupo kama angekuepo ningetamani nimkaribishe sina tatizo naye".


No comments

Powered by Blogger.