Mwana FA atoa sababu mbili za kugombea Ubunge
Mgombea Ubunge Jimbo la Muheza kupitia CCM, Hamisi Mwinjuma maarufu kama MwanaFA, amesema kuwa amesukumwa kugombea jimbo la Muheza kutokana na kero mbili kuu ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ni tatizo sugu kwa wananchi ambazo ni changamoto ya maji na barabara.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa fomu, amesema kuwa barabara ya Muheza hadi Amani yenye urefu wa kilometa 35 ambayo ipo katika kiwango cha changarawe ambayo kwa kipindi cha mvua huwa haipitiki, itakuwa ni kipaumbele chake katika utekelezaji wa majukumu yake.
"Watu wote tunajua kuwa Muheza kuna tatizo la maji, kwa mara ya kwanza nilikutana na mama mmoja akinionesha kichwa chake kimenyonyoka nywele akaniambia ni kwasababu ya kubeba maji, na pili wenzetu wa Amani wanapata tabu sana kwenye kipindi cha mvua barabara haipitiki", amesema Mwana FA.
Kuhusu maslahi ya wasanii amesema "nitahakikisha ninatetea mahitaji ya wasanii kwa ujumla nikiwa bungeni, nitakuwa mmoja kati ya watunga sheria,hivyo wasanii sitawaangusha".
No comments