MAKUBWA...Sauti ya Marehemu Yasikika Wakizika
WALA siyo uongo bali ni kweli kabisa imetokea! Shay Bradley kutoka Leinster, Ireland amezua taharuki muda mfupi baada ya kuzikwa katika Makaburi ya Kilmanagh, ghafla sauti yake ikasikika.
Unajua ilikuwaje? Siku ya mazishi ya Bradley ndugu na marafiki zake wakiwa katika harakati za kuhifadhi mwili wake sauti hiyo ikasikika ikisema;
“Jamani nitoeni nje naogopa huku kuna giza.”
Mbali na kusikika sauti hiyo ya marehemu Bradley, kishindo cha sauti ya jeneza kugongwa kiliendelea huku sauti ile ikilalamika;
“Nitoeni humu kuna giza. Namsikia mchungaji au mimi ni Bradley ndani ya jeneza?”
Jambo hilo liliwafanya watu kutahamaki na kila mmoja wao kutafuta sehemu ya kukimbilia, lakini sauti iliendelea kuzungumza nao;
“Jamani habari zenu ndugu, jamaa na marafiki, mimi nilitaka kuwaambia tu kwaherini.” Kimya ghafla kilitawala.
Inaelezwa kuwa, Bradley alifariki dunia Oktoba 8, mwaka huu na kuzikwa Oktoba 12 ambapo alikuwa akiugua kwa muda mrefu.
Kabla hajafariki, Bradley alitengeneza sauti hiyo ili iwe kichekesho siku ya mazishi yake. Katika ufafanuzi uliokuja kutolewa baada ya mazishi na mtoto wake anasema kuwa;
“Baba alipenda kujua ni watu wangapi angewachekesha siku ya mazishi yake. Hakika baba alikuwa mtu wa ajabu sana, pumzika kwa amani baba. “
No comments