Bayern Munich mabingwa ligi ya Ulaya
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamika leo wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda bao 1-0 mbele ya mabingwa wa Ufaransa PSG.
Fainali hiyo ilichezwa Uwanja wa Da Luz, Lisbon Ureno ilikuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu ilikuwa inahitaji kutwaa ubingwa huo ili kufikia malengo ambayo ilijiwekea awali.
Bao pekee lililoipa ubingwa Bayern Munich lilipachikwa dakika ya 59 na staa wa Bayern Munich ,Kingsley Coman aliyepachika bao hilo kwa kichwa lilidumu mpaka dakika ya 90 huku PSG wakiwa hawaamini wanachokiona.
Bayern Munich ilikuwa bora kuliko PSG kwenye mchezo wa fainali kwani walimiliki mpira kwa salimia 62 huku PSG ikiwa ni asilimia 38 na kwa upande wa mashuti, Bayern ilipiga jumla ya mashuti 12 huku PSG wakipiga mashuri 10, pasi Bayern ilipiga jumla ya pasi 515 huku PSG ikipiga jumla ya pasi 322.
Jitihada za staa wa PSG Neymar hazikuzaa matunda kwani mbinu zote alizotumia kutaka kuipa bao timu yake ziligonga mwamba jambo lililomfanya amwage machozi muda mwingi baada ya kushuhudia timu yake inakosa ubingwa na yeye mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa ni mwaka 2015 wakati huo akikipiga ndani ya Klabu ya Barcelona.
No comments