Header Ads

Header ADS

Wazuri Hasunga "Kinachofanyika HADI Sukari Inaadimika ni Uhuni Mkubwa"



Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Serikali haifahamu kwanini sukari imeendelea kuadimika katika baadhi ya maeneo nchini kwakuwa bidhaa hiyo ipo kwa wingi

Amesema, hakuna uhaba wa sukari Tanzania na kinachofanyika ni uhuni. Ameongeza kuwa kuanzia Jumatatu ijayo, wameandaa mkakati wa kusaka inapofichwa na wataanzia jijini Dar na kisha kwenda mikoa yote nchini

Waziri Hasunga amenukuliwa akisema, "Hatujui kwa nini sukari iuzwe bei ya juu, wakati ipo ya kutosha, tutapita duka kwa duka kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa kubaini wale wote wanaoleta fujo kwenye bidhaa hii"

No comments

Powered by Blogger.