Rais Magufuli Amesema Hivi Karibu Atafungua Shule za Msingi na Chekechea
Rais John Magufuli amesema ugonjwa wa Corona umeisha hivi karibuni atafungua shule za msingi na chekechea.
Rais Magufuli amesema baada ya kufungua vyuo anaangalia hali inavyokwenda ili aweze kufungua vyuo na mwalimu kuendelea kufundisha.
Amesena ugonjwa wa Corona kwa sasa umepungua na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemueleza Dar es Salaam ina wagonjwa wanne.
“Walisema maiti zitazagaa Afrika walikuwa wanatutabiria hawajui kuna Mungu tuliomba siku tatu Corona imeisha nilikuwa napata taarifa kwa Waziri ameniambia Dar ilikuwa na wagonjwa wanne lakini uzushi utatolewa wa kila aina,”
Aidha, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa makini na watu wanaotoa msaada wa barakoa zisije kuwasababishia maambukizi.
No comments