Header Ads

Header ADS

Waziri wa Zamani wa Marekani Colin Powell Asema TRUMP 'Hakufuata' Katiba



Waziri wa zamani wa mambo ya nje ya Marekani Colin Powell amekosoa vikali rais Donald Trump kwa jinsi anavyoshughulikia maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi akisema kuwa "amejipinda" kutoaka kwa katiba.

Mfuasi huyo wa chama cha Republican, na afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani ni wa hivi punde kumkosoa Bw. Trump, kufuatia vitisho vyake vya kutumia majeshi kuvunja maandamano yanayoendelea nchini humo

Amesema atampigia kura mgpombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Kwanini niliamua kutoitazama video ya mauaji ya George Floyd
Mtizamo wa maisha ya Mwafrika anayeishi Marekani
Rais Trump alijibu kwa kumtaja Powell kuwa mtu aliyepewa "hadhi ya juu kuliko anavyostahili".

Bw. Powell, ambaye ni Mmarekani mweusi wa kwanza kuhudumu kama , amejiunga na orodha ya wakuu wa zanmaniwa ngazi ya juu jesheni kumshambulia rais Trump.

Hatua yake inakuja baada ya maandamano ya kitaifa ya zaidi ya wiki moja kupinga ubaguzi wa rangi na dhulma za polisi dhidi ya wananchi zilizosababishwa na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi mjini Minneapolis Mei 5.

Siku ya Jumapili , wanachama tisa kati ya 13 wa bara za la jiji laMinneapolis waliahidi mbele ya mamia ya waandamanaji kuwa watavuja kitengo cha polisi cha mji huo na kubuni kingine kipya "mfumo mpya wa wausalama wa umma ambao utahakikishia usalama jamii yetu".

Huku hayo yakijiri, mikakakati ya kiusalama iliyokuwa imewekwa kote nchini Marekani kufuatia maandamano hayo imelegezwa.

Mji wa New York imeondoa agizo la kutoytoka nje iliyokuwa imewekwa kwa wiki moja, huku Bw.Trump akisema kuwa ataagiza kikosi maalimu cha ulinzi wa kitaifa kuanzo kuondoka kaytika mji wa Washington DC.


Akizungumza na kituo cha habari cha CNN Bwana Powell alisema: "Tuna katiba. Na tunastahili kuifuata. Na Rais ametoka kwenye mkondo wa katiba ."

Akimuashiria Rais Trump, jenerali huyo mtaafu malisema: "Anadanganya kuhusu masuala kadhaa, na kuponyoka kwasababu watu hawamwajibishi ."

No comments

Powered by Blogger.