RC Arusha Ataka Kuipandisha Timu ya Mpira ya Arusha FC Ligi Kuu
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Iddi Kimanta amesema atahakikisha anashirikiana na wadau mbalimbali ili kuisaidia timu ya Arusha FC iweze kufikia malengo yake katika kucheza Ligi Kuu soka Tanzamia Bara.
Kimanta alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa band mpya ya Wisdom Musica, ambapo alisema atahakikisha michezo kwa ujumla kwa kuanza na mpira wa miguu, mpira wa pete ambao nao unasuasua, kadhalika riadha yote ataisimamia ili iweze kuwa katika kiwango bora.
No comments