Header Ads

Header ADS

Rayvany Kutimka WCB Ataja Label Atakayoelekea



Msaani wa Label WCB Wasafi Rayvany ameweka wazi kuwa hawezi kutoka ndani ya label hiyo kwenye maisha yake yote ya kimuziki kwakua label hiyo ni kila kitu kwake.

Akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na redio ya Wasafi Fm Rayvany amesema kuondoka ndani ya wasafi ni kitu kigumu kwake kwakua label ndiyo imemtambulisha kwenye muziki.

“Kwanza kabla sijajibu kwamba ni label gani nyingine naweza kufanyia kazi niseme wazi tu mimi na WCB ni maisha yote nadhani hapo nitakuwa nimemaliza” amesema Rayvany.

Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni Rayvany alikuwa anahusishwa na kuondoka kwenye label hiyo inayooongozwa na msanii Naseeb Abdul (Diamond Platnumz).

No comments

Powered by Blogger.